Iran imemnyonga mwanamke ambaye inadai alimuua mwanamme mmoja ambaye alijaribu kum'baka.
Vyombo vya habari nchin humo vinasema kuwa Reyhane Jabbari aliyekuwa na miaka 26 alinyongwa leo Jumamosi .Inaripotiwa kuwa madai yake kuwa alimuua mwanamume huyo miaka saba iliyopita akijaribu kujilinda yalikosa ushahidi mahakamani ambapo alipatikana na makosa ya kuuwa.
Shirika la haki za kibinaadamu Amnesty International limesema kuwa uamuzi huo ni wa kusikitisha.
Kampeni ilioanzishwa ili kuzima hukumu hiyo katika mitandao ya facebook na Twitter mwezi uliopita haikufua dafu.