Mwanafunzi mmoja aliyetambulika kwa jina la ISAKA SHABAN ALI umuri haujafamika mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya Uhongozaji wa vyombo vya Majini (MASTER FISHERMAN), wa chuo cha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mbegani campas amekufa maji wakati akiogelea katika Bahari ya Hindi. Tukio hilo lilitokea jana, majira ya saa 11 jioni wakiwa katika fukwe ya Mbegani Bagamoyo.
Kwa mujibu wa shuhuda waliokuwa eneo la tukio walidai, Isaka alifika na wenzake katika fukwe hiyo kwa lengo la kufanya mazoezi.
Ndipo wakati wakiogelea alizidiwa na maji na kuzama kwaa kunywa maji mengi ndipo wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayali ilikuwa mbaya
Na kukimbizwa kituo cha Afya katika Hospitali ya wilaya Bagamoyo.
lakini jitiada za kuokoa Maisha yake zilishindikana.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAALI PEMA PEPONI AMEN