WASHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza klabu ya TP Mazembe ya Congo,
Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamewasili asubuhi ya
leo tayari kuwavaa Msumbiji (Balck Mambas) jumapili ya wiki hii ndani ya
dimba la Taifa.Mechi
hiyo ni ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki
fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mwakani nchini Morocco na
mshindi wa jumla katika mechi mbili ndiye atafuzu hatua ya makundi.
Nyota hao wametua nchini kwa ndege ya Egypt Air wakitokea Tunisia ambapo timu yao ya TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa
njema kwa mashabiki wa soka nchini ni kuwa washambuliaji hao wenye
uzoefu na mechi za kimataifa wamewasili wakiwa fiti kwa kazi.
Samatta
aliwakosa Zimbabwe mjini Harare, lakini safari hii yuko fiti na
ameahidi kufanya kazi ya kulisaidia taifa katika mchezo wa jumapili.
Pia
shukurani kwa TP Mazembe waliowaruhusu wachezaji hawa mapema kujiungga
na wenzao, hivyo ni matarajio ya kuwaona nyota hao wakisaidiana na
wenzao kuifunga Msumbiji nyumbani.
Taifa
stars inahitaji ushindi wa zaidi ya magoli matatu katika uwanja wa
nyumbani ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo
wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye mjini Maputo nchini
Msumbiji.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi Tukuyu
mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi
Mahmoud Ashour kutoka Misri.
Stars
itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwa
ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku hiyo hiyo.
Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini
Msumbiji