Kama unaweza kushiriki maombi haya pamoja nami, Mungu akukumbuke, na
kama upo kwa ajili ya kuhukumu, pia Mungu akukumbuke. Math7:1 Msihukumu
msije mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo
hukumuwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakacho pimiwa.
Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
‘ Mungu wewe ni Mtakatifu,
Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe ni mwanzo tena mwisho
zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema ktk 1wathesalonike5:18
shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu ktk kristo
Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana yangu, leo na kesho
itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi yangu, mwili wangu na
roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.
Ktk Isaya43;19
umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je hamtalijua
sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani. BWANA
mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk
Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya.
ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu
haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.
Maombolezo3:31-32 Kwa kuwa
BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo mhuzunisha atamrehemu kwa
kadiri ya wingi wa huruma zake.
Mungu inua moyo wangu sasa,
wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama
ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana
ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
ninashuka mbele zako ninaungana na wenye uhai wanne
ktk Ufunuo4;6-11 kukuabudu wewe nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu
na MUNGU wetu,kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe
ndiwwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako
navyo vikaumbwa.
Zab23;4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.
AMEN