Tukio hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi minane na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama yake mdogo.
Baada ya kufika kwa mama yake mdogo aliomba maji kwa ajili ya kwenda chooni, hata hivyo alizunguka nyuma ya choo kwa ajili ya kujipa msaada wa siri lakini hali ilivyokuwa mbaya zaidi, aliamua kuingia ndani ya choo hicho na kujifungua kichanga hicho na kukidumbukiza ndani ya shimo la choo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walimuona mwanamke huyo akibebwa kwenda ndani kwa mama yake mdogo ili aweze kupatiwa msaada zaidi lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa kuanza kuvimba mwili kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Waandishi wetu walifanikiwa kuzungumza na mama mdogo wa mwanamke huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la mama Athony alikiri binti huyo kukumbwa na mkasa huo wakati yeye akiwa kwenye shughuli zake.
“Kweli nafahamu, alikuwa ni mjamzito na alifika nyumbani kwangu saa tano asubuhi, alichokifanya hapa si kitu cha bahati mbaya ni makusudi,” alisema mama huyo.
Mama Antony alisema kuwa wakati anarudi nyumbani aliukuta umati wa watu na alipoingia ndani ndipo alipopewa habari za tukio hilo.
Alipotakiwa kutaja jina la binti huyo, mama huyo alianza kuangua kilio na kuwafanya waandishi wetu washindwe kuendelea na mahojiano naye.
Mwakilishi wa mjumbe na shina namba 34 Ukonga Mazizini, Bi Mtende alisema kuwa tukio hilo limewashangaza kutokana na mwanamke huyo kwenda kutupa kichanga chooni kwa makusudi.
Bi Mtende alisema kwanza mwanamke huyo siyo mkazi wa maeneo hayo, hivyo hakuna aliyeweza kumjua kwa jina.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika katika eneo hilo majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutimiza wajibu wao
Kikosi hicho kikiwa kimesheheni zana za uokoaji kilikuta kichanga hicho kikielea chooni na kwa kutumia mbinu zao za uokoaji na walifanikiwa kukitoa kichanga hicho kikiwa kikiwa maiti.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo yeye aliliita ni la kikatili na mwanamke huyo amepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na mwili wa kichanga hicho kimepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Waandishi wetu walifika katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya kupata mahojiano na mama huyo Jumanne iliyopita, hata hivyo