Leo tarehe 28 Aprili 2012, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager
amemtambulisha kwa waandishi wa habari, Mhariri wa habari za burudani wa
gazeti la mwananchi, Bw Henry Mdimu kuwa msemaji mkuu wa Academy ya
Kili Music Awards kwa msimu huu wa mwaka 2013/14 katika ukumbi wa safari
Pub uliopo ilala, katika bohari ya kampuni ya bia Tanzania, TBL
Mdimu ambaye amekuwa Mjumbe wa Academy kwa mwaka wa nne sasa, pia mwaka
jana aliongoza jopo la majaji katika kutafuta vipaji vipya vya muziki wa
kizazi kipya, katika ziara iliyoitwa Kili Talent search Tour ambapo
wasanii kama Yopung Killer na neylee walipatikana kupitia msako huo
ulioendeshwa katika mikoa mitano.
Uteuzi wa mdimu umepokelewa kwa mtazamo chanya na wadau huku kila mmoja
akiamini uchapakazi wake na uadilifu alionao katika medani ya sanaa ndio
uliopelekea mpaka Baraza la sanaa la taifa, ambao ndio wamiliki halali
wa tunzo hizo, kulitaja jina la mdau huyu ambaye mwaka huu ametimiza
miaka 17 tangu kuanza kazi ya uandishi wa habari za burudani.
Mdimu ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Times,
baada ya uteuzi huo alionekana akiwa mtu mwenye kuangalia uwezekano wa
kuirasimisha fani ya muziki kuwa ajira rasmi yenye kuheshimika.
"Hili ni daraja nimepandishwa, lakini nataka kuwaambia ndugu zangu
kwamba nitaitumia hii nafasi kama jukwaa la kusemea wasanii wetu wa
Tanzania, ili wafikier hadhi zao ambazo mpaka sasa, wengi wao
hawajazitambua".
Mdimu ambaye ni mjukuu wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya
Watangatanga, Mzee Herry Mdimu ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja na
mwakani atachaguliwa msemaji mwingine>
Home
»
»Unlabelled
» HENRY MDIMU ATEULIWA KUA MSEMAJI WA KILL MUSIC AWARDS
Topics:
Imehaririwa na;- poatel Africa
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea ...
-
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri huyo amba...
-
KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye len...
-
Huu ndo ujio mpya Rehema Chalamila aka Ray C baada ya ukimya wa muda mrefu kwenye muziki amerudi rasmi na hii singl...
-
Hivi karibuni mdau mmoja wa Website hii alinitumia e-mail na kuniuliza ni kwa jinsi gani anaweza kuipata simu yake iliyo...
-
Kampuni moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom Ship’, itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu ch...
-
Makala hii inakupa maelekezo ya mambo adimu katika kusimamia barua pepe zako, ili kuboresha ufanisi na- kufurahia kuwa na akaunti ya ema...
-
Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa ...
Data Boosta
