Header ads

Header ads
» » Zifahamu Mashine za uchapishaji wa 3D zinazoweza kuchapisha vyakula


Tukizungumzia mashine ya kuchapisha vyakula, kwanza tunahitaji kutaja teknolojia ya uchapishaji wa 3D.
Mwaka 1986 Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Marekani kilivumbua mashine ya kwanza ya uchapishaji wa 3D, baadaye teknolojia hii ilipata maendeleo ya kasi na kutumiwa katika kazi mbalimbali.
Mwaka 2011, watafiti wa Uingereza walisanifu mashine ya kwanza ya kuchapisha chokoleti. Baadaye kampuni ya Hispania iliboresha teknolojia yao na kutengeneza mashine ya kuchapisha chakula iitwayo Foodini. 


Ready made: The design takes the form of a set of syringes that deposit food inks line by line, and layer by layer, according to an electronic blueprint Siku hizi mashine za uchapishaji wa 3D zinaweza kuchapisha zaidi ya aina 30 ya vyakula, vikiwemo chokoleti, pipi, jeli, biskuti, keki, chipsi, jamu za matunda au mboga, vyakula vyenye nyama, jibini na mtindi. Mashine ya kwanza ya uchapishaji wa 3D wa vyakula ni ya kuchapisha chokoleti, na pia ni mashine inayopata maendeleo ya kasi zaidi.

Teknolojia ya kuchapisha vyakula inasaidia kutoa vyakula tofauti kwa mujibu wa watu mbalimbali wakiwemo watoto na wazee. Kampuni moja ya Ujerumani imezalisha chakula kiitwacho "Smooth food" ambacho ni rahisi kutafunwa na kumezwa. Chakula hiki huenda kitatumiwa kwa wingi katika kazi ya kuwatunza wazee.
Aidha, teknolojia hii inawawezesha watu kuchapisha vyakula vipya kwa kutumia lishe za mwani, majani ya viazi sukari na wadudu, ili kutatua tatizo la ukosefu wa chakula duniani. 


Chanzo: dailymail.co.u

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post