Header ads

Header ads
» » » Mtandao wa 4G wavunja Rekodi ya kasi katika simu


Kampuni ya Finland Elisa inasema imefanikiwa kupata kasi ya Gigabait 1.9 kwa sekunde, ikisema hiyo ndio kasi ya juu zaidi kuwahi kupatikana.
Huduma hiyo ya simu yenye kasi zaidi inaweza kupakua Filamu ya Blu Ray kwa muda wa sekunde 44.
Lakini wachanganuzi wana wasiwasi kwamba kasi hiyo inaweza kutumika moja kwa moja katika mtandao halisi ulimwenguni.
Elisa imesema kuwa imetumia teknolojia iliotolewa na kampuni ya China ya Huawei kutoa kasi ya upakuzi katika mtandao wa simu uliokaribia kiwango cha 2Gbps .
Ukilinganisha kasi yake ya mtandao ni 300Mbps ambayo iko chini mara sita.
Mkurugenzi mkuu Veli -Matti Mattila amesema: Tunajua kwamba hakuna kasi kama hii iliotangazwa na mitandao mingine. 

Chanzo: brecorder.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post