Header ads

Header ads
» » MakiniApp:#APP ya kuzuia ajali zisababishwazo na mwendokasi Barabarani

Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Makini Road Safety Foundation imeturahisishia njia nyepesi ya kukabiliana na ajali za barabarani ambapo kwa kutumia application ya MakiniApp ambayo ukiwa nayo katika simu yako, itakusaidia kujua mwendokasi wa dereva kwenye gari ulilopanda.


TeknoTaarifa inatoa Pongezi za dhati kwa Jeshi la Polisi - Kitengo cha Usalama Barabarani kwa kutokomeza ajali zisababishwazo na mwendokasi kwa kuzishughulikia taarifa zinazotumwa na watumiaji wa #Makiniapp.
Ewe mdau,Download Makiniapp ili uweze kuitumia ukiwa safarini na uweze kutambua pindi dereva anapoendesha kuzidi kikomo cha mwendokasi cha barabara husika.
Kwa pamoja tunathubutu kutokomeza ajali zisababishwazo na mwendokasi. 

Msemaji mkuu wa MakiniApp Irene Kidunda Alisema
"MakiniApp hii ni application ambayo inamuwezesha mtumiaji kufahamu kiwango halisi cha mwendokasi wakati anaoutumia dereva wakati wa safari kupitia simu yake‘ ‘Ikiwa dereva anatembea kwa mwendokasi usiotakiwa mtumiaji anaweza kuchukua hiyo taarifa na kuituma katika kikosi cha usalama barabarani kupitia hiyohiyo simu yake ili askari wamchukulie hatua dereva huyo"
Aliendelea kusema
"Uzuri wa kuwa na application hii ni kwamba hatakama hutakuwa na mtandao kwa muda huo bado utakuwa na uwezo wa kurekodi mwendokasi wote na kisha ukampatia askari polisi utakayemkuta barabarani na bado ikawa na msaada"

JESHI LA POLISI LAZINDUA APP KWA AJILI YA KUZUIA AJALI ZA BARABARANI YA MAKINI APP
MakiniApp imerasimishwa kua application pekee Tanzania itakayotumika na jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa ajili ya kupokea taarifa za mwendokasi zitakazokua zikitumwa na abiria wa vyombo vya moto (pikipiki na motokaa) waliotumia MakiniApp ili kuepeusha ajali zisababishwazo na mwendokasi.
- Taarifa itakusanywa na MakiniApp.
- Itatumwa kwa namba ya simu ya jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani  (0682 88 77 22 - ambayo imeunganishwa na mitandao ya kijamii yaani Whatsapp na Telegram na kufanyiwa kazi mara moja.
Kwa pamoja tushirikiane kutokomeza ajali za mwendokasi kwa kuhimiza matumizi ya MakiniApp ili tupeleke taarifa za mwendokasi zilizo na vithibitisho.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post