Header ads

Header ads
» » Njia mbadala za kuhifadhi Taarifa (Faili) zako Mtandaoni



Uzuri wa Teknolojia ni kwamba kama uko makini basi hutaweza kupoteza taarifa zako zozote ambazo zipo katika vifaa vyako kama vile simu na kompyuta…
Taarifa hizo zinaweza zikawa katika mfumo wa picha, video, sauti na kadhalika.  

Hizi ni njia mbili ambazo unaweza ukatumia katika kuhakikisha unahifadhi mafaili yako katika mtandao
1. Kwa Kutumia Google Drive

 http://www.mobipicker.com/wp-content/uploads/2016/06/google-drive.jpg
Hapa haijalishi unataka kuhifadhi kitu gani, kuanzia video, sauti, picha n.k vyote utaweza kuvihifadhi humu. Huduma hii ukijiunga nayo kwa mara ya kwanza inakuwa ujazo wa GB 15 za bure ambazo unaweza ukazijaza kwa kuhifadhi mafaili yako. Kwa haraka haraka GB 15 ni sawa na nyimbo 4,000 (kwa makadirio)
Ukihifadhi taarifa (mafaili) yako katika Google Drive basi pale tuu utakapokuwa na kifaa chenye intaneti utaweza kuyapata mafaili yako. Yaani kwa mfano kama simu yako imeisha chaji na mafaili yako yapo katika Google Drive basi unaweza ukayapitia kwa kutumia kompyuta yeyote yenye intaneti.
Uzuri wa Google Drive ni kwamba kila mtu mwenye account ya Google (Gmail) basi anaweza akatumia huduma hii
Google Drive
Unaweza amua kuaangalia vitu vyako humo humo katika Google Drive au ukaamua kuvishusha katika kifaa chako. Kwa mfano kama kuna muziki umeuhifadhi humu una uwezo wa kuucheza humo humo (kama una intaneti) au ukaamua kuushusha katika kifaa chako.
Ili kuitumia ingiza taarifa zako za Gmail ambazo ni barua pepe (e-mail) na password (nenosiri).ukishafanikisha hilo basi unaweza ukaanza hifadhi mafaili kwa kubofya katika alama ya +. Unaweza ukapandisha mafaili mengi unavyotaka ili mradi yasizidi kile kiwango cha GB 15. Kama ukiona yanazidi basi unaweza ukaamua kuhamishia mafaili hayo katika kompyuta au katika ‘hard disk’ ya nje
Kwa watumiaji wa iOS wanaweza kuipakua hapa!
Kwa watumiaji wa Android wanaweza kuipakua hapa!
Kwa kutumia kompyuta unaweza ukaipata kwa kuingia >> Drive.Google.com
 

2. Kwa Kutumia Dropbox
Dropbox
Dropbox haina tofauti kubwa sana na Google Drive. Dropbox yenyewe inatoa ujazo mdogo wa bure wa uhifadhi ambao ni GB 2. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea mtandao wao (www.Dropbox.com) na uingize taarifa zako za muhimu ili kujiunga na huduma hii
Ukishafanikisha hilo basi unaweza ukaanza hifadhi mafaili kwa kubofya katika alama ya +. Unaweza ukapandisha mafaili mengi unavyotaka ili mradi yasizidi kile kiwango cha GB 2.
Dropbox
Kumbuka GB 2 ni ndogo sana, hapa inakubidi uwe na tabia ya kuhamisha vitu mara kwa mara katika kompyuta yako au ‘hard disk’ ili mradi kuhakikisha kuwa ujazo huo haujai. Ila pia Dropbox wanaweza kukuongezea kwa kila unapoalika watu wengine katika huduma hiyo.
Kwa watumiaji wa iOS wanaweza kuipakua hapa!
Kwa watumiaji wa Android wanaweza kuipakua hapa!
Kwa kutumia kompyuta unaweza ukaipata kwa kuingia >> https://www.dropbox.com/
Najua wengi tumezoea kuchemeka USB na kuunganisha simu janja na kompyuta zetu ili kupata mafaili tunayotaka kuyahamisha lakini zoezi hili ni rahisi sana kwa kutumia uhifadhi wa mtandaoni. Na pia kama nilivyosema unaweza ukaibiwa hicho kifaa chako na taarifa zote zikapotea tena hasa hasa kama wewe ni mmoja kati ya wale ambao hawahifadhi taarifa zao katika mtandao 


Chanzo na Marejeo: thenextweb.com & mobipicker.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post