Header ads

Header ads
» » » Huyu ndiye Mwanaume aliyefunga ndoa na simu yake


Tumeshasikia na kuona vioja vingi duniani, lakini kioja hiki kimekuwa cha kipekee au cha mwaka kama waswahili wasemavyo.
Si kawaida kwa sisi watanzania kusikia mtu kaoa au kaolewa na kitu kisicho na uhai, lakini kwa nchi za wenzetu hili limekua jambo la kawaida sana, mwanaume kuoa gari au mwanamke kuolewa na joka.
Hivi karibuni kule nchini Marekani mwanamume mmoja anayetambulika kwa jina la Aaron Chervenak aliamua kuonesha upendo wake wa dhati kwa simu janja yake (Smartphone) alipoamua kufunga nayo ndoa.

Aaron alifika katika mji maarufu kwa Kamari nchini Marekani  wa Las Vegas na kutafuta kanisa litakaloweza kuhalalisha ndoa yake na simu janja ambapo alielekea katika kanisa moja lijulikanalo kama The Little Las Vegas Chapel, ambapo alikutana na mmiliki wa kanisa hilo na kumweleza shida yake.
Screen Shot 2016-07-08 at 2.00.14 PM
Aaron alimweleza mmiliki huyo wa kanisa kuwa alikua na uhusiano na simu yake kwa kipindi kirefu sasa, na ndio maana anataka kufunga nayo pingu za maisha.
Mmiliki wa kanisa hilo alistushwa na uamuzi wa Aaron, lakini baadae aliona ni sahihi kwa Aaron kufunga pingu za maisha kwa kitu akipendacho. Mmiliki wa kanisa alikiambia  kituo cha tv cha KTNV
Happy together? Aaron can be see looking lovingly at his smartphone during the one-of-a-kind ceremony  

The bride wore white! Aaron dressed his black iPhone in a special case for the event 
Mnamo Tarehe 20 Mei, Aaron alifika kanisani na kuweka historia ya kuwa mwanamume wa kwanza duniani kufunga pingu za maisha na simu janja (Smartphone), Japokuwa kitendo hicho hakitambuliwi na Jiji hilo la Nevada.
Screen Shot 2016-07-08 at 2.03.43 PM
Katika maisha ya Mtanzania wa kawaida, simuni kitu ambacho huambatana nacho popote aendapo, wengine wanadiriki kuingia na simu zao hata chooni ili kujiliwaza wakiwa katika haja huku pia simu ikiwa ni kitu cha mwisho kukitazama kabla ya kulala na kitu cha kwanza kutazama uamkapo, Je, hizo ndizo sababu pekee za kukufanya ufunge ndoa na simu? 

Chanzo: dailymail.co.uk

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post