Header ads

Header ads
» » Vitu muhimu vya kuangalia unapotaka kununua kompyuta


1. Kiendeshi diski kuu (Hard Disk):
Diski kuu au kiendeshi diski kuu ni sehemu ya kompyuta ambako kumbukumbu ya habari hutunzwa. Inaitwa pia kwa kifupi chake cha Kiingereza HDD (hard disk drive) au HD (hard drive). Inaitwa diski kuu kwa sababu kompyuta hutumia diski mbalimbali kwa mfano CD, flash disk au diski ndogo aina ya flopi.
Kwahiyo kiendeshi diski kuu au hard disk drive kwa lugha nyepesi ni memori kadi ya kompyuta. Zina ukubwa tofauti tofauti kutegemea na mahitaji na malengo ya mwenye kompyuta. Ukubwa wa HDD hupimwa katika jigabaiti (GB) na siyo umbile lake. Programu nyingi za kompyuta za kisasa zinahitaji HDD zenye ukubwa kuanzia GB 160 na kuendelea, nakushauri kama una uwezo ununuwe kompyuta yenye hard disk kuanzia gb 500 na kuendelea.

Muundo wa HDD:
Diski kuu kwa kawaida inaonekana kama kisanduku kidogo cha metali iliyofungwa kabisa. Ndani yake kuna diski inayotunza kumbukumbu na data zote zilizowekwa katika Kompyuta. Kisanduku hicho kimefungwa kabisa ili vumbi au takataka visiweze kuingia ndani yake.Ndani ya sanduku ya nje kuna diski nyembamba au kisahani kimoja, viwili au zaidi. HDD Zinatengenezwa kwa kioo au aloi ya aluminiamu. Diski hii imefunikwa kwa ganda la aloi lenye tabia ya kisumaku.

Kazi za HDD katika kompyuta:

(a) Kuandika;
Diski huzungushwa kwa injini ya umeme ndogo haraka sana hadi mara 15,000 kwa dakika. Mkono unaoshika kalamu sumaku (huitwa pia “head” – kichwa) unapita juu yake. Kalamu inaacha alama sumaku kwenye mahali padogo usoni mwa diski. Mfululizo wa nukta zenye chaji na nukta bila chaji zinatunza habari kwa mfano wa herufi za alfabeti au pia picha. Chaji hubaki mahali pake kutokana na sifa za aloi inayofunika diski.

(b) Kusoma;
Wakati wa kusoma habari/data mkono unapita juu ya uso wa diski na kalamu inafanya kazi kinyume ya kuandika, safari hii inagundua alama sumaku zilizopo na mfululizo wa nukta sumaku na nukta bila alama ya sumaku unasomwa na tarakilishi.

(c) Kufuta;
Wakati wa kufuta kumbukumbu mkono unapita juu ya sehemu ya diski ambako habari inatakiwa kufutwa na kuondoa chaji.
Unashauriwa kutokuweka sumaku karibu na kompyuta kwa sababu sumaku inaweza kuathiri kumbukumbu kwenye diski.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post