Header ads

Header ads
» » TCRA imeziagiza kampuni za simu kutenganisha vifurushi


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeziagiza kampuni za simu kuanzisha vifurushi vinavyotenganisha huduma za inteneti, sauti na meseji ili kuwapatia machaguo wananchi na kuwapunguzia gharama zisizo za lazima.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba amesema hayo wakati wa ufunguzi wa semina kwa walimu wa uziwi.  Agizo hilo lililowahi kutolewa awali mapema mwaka huu litafanya kampuni hizo kuweka vifurushi rafiki kutokana na mahitaji ya mtumiaji.
Hatua hiyo, kwa mujibu wa mdhibiti huyo, ilitokana na kuwepo malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kushushwa ghafla viwango vya huduma katika vifurushi vingi vya mitandao ya Vodacom, Tigo na Airtel mapema mwaka huu.
“Vifurushi vingi vinajumuisha huduma ambazo baadhi ya watumiaji hawahitaji. Mfano, mtumiaji mwenye uziwi anahitaji zaidi kifurushi cha meseji zaidi kuliko sauti. Mtumiaji asiyeona anahitaji zaidi kifurushi cha kuzungumza kuliko meseji.
“Hivyo mamlaka imeagiza kampuni kuvitenganisha vifurushi kwa mahitaji ya mtumiaji,” amesema Dk Simba.
Amesema baada ya agizo TCRA imekuwa ikifuatilia kwa karibu utekelezaji wake na kwamba baadhi ya kampuni zimeshaanza kutenganisha vifurushi hivyo kama ilivyoamriwa.
Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa Sheria ya kudhibiti uhalifu mtandaoni ya mwaka 2010, Dk Simba amesema kuwa TCRA imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka jeshi la polisi kutoa ushahidi wa kesi mbalimbali zinazohusu uhalifu mtandaoni.
Amesema katika utekelezaji wa sheria hiyo iliyoanza Septemba Mosi mwaka huu, wamekumbana na changamoto ya baadhi ya watu kukosea na kupeleka malalamiko yao moja kwa moja TCRA badala ya polisi ambao wana mamlaka ya kisheria kufungua kesi za jinai.
“Tangu kuanza kwa sheria hiyo nidhamu ya matumizi ya mtandao imeanza kuimarika japo wapo baadhi wanaendelea kuvunja sheria. Hata hivyo, kumbuka hata tukipata ushahidi ni suala la polisi kuendelea au kutoendelea na kesi,” amesema Dk Simba.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post