Header ads

Header ads
» » Simu mpya ya LG Nexus 5 kutambulishwa rasmi tarehe 29 Septemba mwaka huu

LG Nexus 5 kuzinduliwa mwezi huu

Kampuni ya LG imetangaza kwamba itatambulisha rasmi simu yake mpya ya LG Nexus 5 kwenye maonyesho ya teknolojia yatakayoandaliwa tarehe 29 Septemba mjini San Francisco.
Katika maonyesho hayo,simu nyingine mpya zilizoundwa kwa ushirikiano wa LG na Huawei pia zitatambulishwa.
Muonekano pamoja na maelezo ya kiufundi kuhusiana na LG Nexus 5 yalivujishwa mtandaoni na vyanzo vya karibu vya kampuni ya LG.
Kwa mujibu wa muonekano na maelezo hayo, LG Nexus 5 itakuwa na kamera mbili za Flash LED zenye ubora wa 13 MP kama ilivyokuwa katika simu ya LG G3.
Simu hizo pia zitakuwa na sehemu ya king’amuzi cha kutambua alama ya kidole, skrini ya QHD yenye upana wa inchi 5.2, mfumo endeshi wa Snapdragon 808, RAM ya 3GB na kutumia mfumo mpya wa Android.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post