Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, madawa hayo ya kulevya yalikuwa yamefichwa ndani ya viroba 40 na kufunikwa kwa kemikali ya Zinc Oxide kwenye ndege ya shehena aina ya AM0762 inayomilikiwa na shirika la ndege la Copa Airlines.
Video iliyorekodiwa na kamera za siri ilionesha viroba 40 vilivyokuwa na madawa ya kulevya yaliyofungwa ndani ya paketi ndogo za plastiki.
Hakuna mhusika yeyote wa ulanguzi wa madawa ya kulevya aliyetiwa mbaroni katika operesheni hiyo ingawa ripoti zinaashiria kwamba madawa hayo yalitoka kwa walanguzi wa Bogota na Cartagena waliokuwa na uhusiano wa kibiashara na Mexico.
Maafisa wakuu wamearifu kwamba madawa ya kulevya yalipangwa kusambazwa Marekani na Ulaya kupitia Marekani ya Kati.
Mnamo wiki jana, polisi wa Mexico pia waliwahi kukamata kilo 961 za madawa ya kulevya katika operesheni yao.