Header ads

Header ads
» » Microsoft yatangaza kuondoa baadhi ya programu za vifaa vya Lumia

Habari mbaya kwa watumiaji wa vifaa vya Lumia

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft imetangaza kuondoa baadhi ya programu zake zilizokuwa zikitumika kwenye vifaa vya Lumia.
Microsoft iliyobainishwa mpango wake wa kuondoa programu 7, imesema kwamba itaondoa programu 5 kwa sasa, kisha baadaye itaondoa nyingine 2 zilizobaki.
Microsoft inadaiwa kuchukuwa hatua hiyo ili kuboresha muonekano wa picha kwenye mfumo wa Windows.
Miongoni mwa programu zilizoondolewa kwa sasa ni Lumia Storyteller, Lumia Beamer, Photobeamer, Lumia Refocus, Lumia Panorama na Video Uploader.
Hata hivyo baadhi ya programu kama vile Lumia Panorama na Video Uploader, zinaarifiwa kwamba zitaendelea kufanya kazi ingawa hazitofanyiwa usasishaji wala maboresho.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post