Header ads

Header ads
» » Hifahamu Afya ya kisaikolojia au kiakili anayokuwa nayo mtu.

Afya ya kisaikolojia

Katika miaka na enzi zilizopita jamii mbalimbali duniani zilijaribu kuelewa hisia na fikra za watu katika jamii na jinsi ya kuwasaidia waliokuwa na fikra au hisia potovu au yenye kuathiri vibaya maisha na afya ya kimwili ya binadamu.
Tangu utotoni binadamu hujifunza au hufunzwa jinsi ya kuepuka magonjwa ya kimwili kwa mfano watoto huhimizwa kuvaa sweta au koti wakati wa baridi, usafi wa mwili, mavazi na sehemu wanayoishi watu huhimizwa sana na pia watu hupokea chanjo ili kujilinda na maradhi. Ili kuzuia magonjwa ya mwili binadamu huchukuwa tahadhari za kila aina. Je, afya ya kisaikolojia inapewa umuhimu sawa?
Watu wengi bado hawajang'amua umuhimu wa kuchunga afya yetu ya kisaikolojia. Magonjwa ya kisaikolojia ni hatari zaidi ya magonjwa yanayoathiri mwili wa binadamu kwa sababu kadhaa. Moja ni kwa kuwa magonjwa ya kisaikolojia ni vigumu kujua unapougua. Pili ni kwamba licha ya kujua kuwa unamatatizo fulani unaweza kuwaficha jamaa zako na marafiki. Tatu ni kwamba matatizo ya kisaikolojia huathiri anayeugua pamoja na wale waliokaribu naye kama vile jamaa na marafiki. Na la nne na la mwisho ni kwamba baadhi ya matatizo ya kisaikolojia huweza kupelekea kuzorota kwa afya ya mwili na hata kumfanya mtu kuchukua hatua ya kujiuwa.
Baadhi ya mambo ambayo humfanya mtu kuwa na matatizo ya kisaikolojia ni matatizo katika familia, upweke na kutengwa, kufeli au kutopata mafanikio uliyokuwa ukitarajia.
Katika makala ya pili tutajadili jinsi vitu hivi vinavyoweza kuathiri afya ya kiakili na hatua tunazoweza kuchukua.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post