Header ads

Header ads
» » Gari mpya aina ya Apple Car itakayotumia umeme kuingizwa barabarani mwaka 2019

 Apple Car kuingizwa barabarani mwaka 2019


Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple kutoka Marekani imepiga hatua kubwa katika soko la magari kwa kuunda Apple Car itakayotumia umeme.
Gari ya Apple Car iliyokuwa ikifanyiwa majaribio kwa muda mrefu, inatarajiwa kuingizwa rasmi barabarani mwaka 2019.
Gari hiyo iliyoundwa katika mradi wa Titan unaojumuisha wahandisi 600 wenye utaalamu wa hali ya juu, inatarajiwa kuvutia wengi kwa muundo wake wa teknolojia ya kisasa.
Ingawa Apple Car inaarifiwa kutumia umeme, bado haijabainishwa iwapo itaendeshwa na dereva au itaweza kujidhibiti yenyewe.
Vyanzo vya karibu vya kampuni hiyo pia vimefahamisha kwamba Apple Car itakuwa na usukani.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post