Header ads

Header ads
» » Bayern Munich kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wahamiaji nchini Ujerumani

 Msaada kwa wahamiaji kutoka kwa Bayern Munich

Mabingwa wa Bundesliga kufungua kambi ya mazoezi na kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wahamiaji nchini Ujerumani

Kilabu ya Bayern Munich imetangaza mpango wake wa kufungua kambi ya mazoezi pamoja na kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wahamiaji nchini Ujerumani.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kilabu ya Bayern Munich, msaada huo wa fedha Euro milioni 1 utasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya wahamiaji.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba wachezaji wa Bayern Munich wataingia uwanjani na watoto wa wahamiaji pamoja na wa Kijerumani wakati wa mechi dhidi ya Augsburg itakayochezwa tarehe 12 Sepetemba.
Bayern Munich pia itatoa misaada ya kifedha, bidhaa na vifaa mbalimbali kwa wahamiaji waliokuwa karibu na mji wa Munich na Bavaria nchini Ujerumani.
Kambi hiyo ya mazoezi inayotarajiwa kufunguliwa katika wiki zijazo, itasaidia kukuza vijana na watoto wa wahamiaji kiafya na kisaikolojia.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post