Header ads

Header ads
» » Msongamano mkubwa wa watu katika sherehe wasababisha vifo India

Msongamano mkubwa wa watu wasababisha vifo India

11 wafariki baada ya kukanyagwa katika sherehe ya kitamaduni iliyoandaliwa kwenye hekalu moja mashariki mwa India

Watu 11 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kukanyagwa katika msongamano mkubwa wa watu waliokuwa wamehudhuriwa sherehe ya kitamaduni iliyofanyika ndani ya hekalu moja mashariki mwa India.
Vifo hivyo vilizuka baada ya maelfu ya watu kusongamana kwenye lango la hekalu walipokuwa waking’ng’ania kuingia ndani nyakati za alfajiri katika mji wa Deogarh ulioko mkoani Jharkhand.
Watu hao 11 waliofariki walikuwa wamelala usiku nje ya lango la hekalu kwa lengo la kuwatangulia wenzao kuingia ndani asubuhi iliyofuatia.
Watu hao wanaojumuisha wanawake 8 walifariki baada ya kukanyagwa na wenzao waliokuja asubuhi, huku wengine 24 pia wakiripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.
Sherehe hiyo ya kitamaduni iliyokuwa na umuhimu mkubwa katika imani ya Wahindi inatarajiwa kuendelea kwa mwezi mmoja.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post