Header ads

Header ads
» » Mshambuliaji mwingine kutoka Mali atua Simba kwa majaribio

 
MSHAMBULIAJI Makan Dembele kutoka Mali amewasili nchini kwa majaribio ya kujiunga na Simba SC. Mchezaji huyo aliwasili juzi jioni na kuungana na Abdoulaye N’daw wa Senegal katika majaribio hayo.
Msemaji wa Simba Haji Manara aliliambia gazeti hili jana kuwa, wachezaji hao wamekwenda Zanzibar kuungana na wenzao walio kwenye kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu. Kwa mujibu wa Manara, N’daw anatoka Dinamo Bucuresti ya Romania na Dembele anatoka JS Kabylie ya Algeria.
Simba imeamua kuleta wachezaji hao n kuachana na Papa Niang wa Senegal aliyeshindwa majaribio. Mchezaji huyo alijaribiwa Jumatatu wiki hii katika mechi dhidi ya Mwadui na kushindwa kuonesha kiwango cha kuridhisha katika dakika 45 alizochezeshwa kwenye mechi hiyo ambayo timu hizo zilitoka suluhu.
“Tumepata wachezaji wengine wawili, mmoja ametoka Senegal tena na mwingine Mali, hao wamefika jana (juzi) na wamekwenda Zanzibar benchi la ufundi litaangalia uwezo wao na kuona nani asajiliwe,” alisema Manara. Kabla ya kuleta wachezaji hao kwa mjaribio, Simba ilikuwa ikiwania kumsajili Laudit Mavugo wa Vital ‘O’ lakini ilishindwa dau.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post