Header ads

Header ads
» » Deni lamponza Chris Brown Azuiliwa kutoka uwanja wa ndege nchini Ufilipino

 Deni lamponza Chris Brown Ufilipino

Msanii nyota wa muziki wa nchini Marekani, Chris Brown amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzuiliwa kutoka uwanja wa ndege nchini Ufilipino

Nguli huyo wa muziki nchini  Marekani alikwenda nchini Ufilipino kufanya onyesho kabambe wiki iliyopita.
Mara baada ya onyesho hilo, Chris alipanga kuondoka nchini humo siku ya Jumatano kwa ndege yake binafsi kuelekea Hong Kong kwa ajili ya onyesho jingine.
Lakini serikali ya Ufilipino ilitoa tangazo kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Manila kutomruhusu Chris kuondoka mpaka atakapolipa deni lake.
Deni hilo amatakiwa kuwalipa wadhamini ambao walimuandalia tamasha kali kipindi cha mwaka mpya, ingawa Chris hakutokea kwenye show hiyo.
Lakini Brown mwenyewe aliandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, "Sijui chochote kuhusiana na mambo yanayotendeka sasa. Nilikuja hapa kufanya onyesho kama malipizo ya onyesho nililolikosa kipindi cha mwaka mpya. Na nimeshafanya onyesho hilo siku tatu zilizopita".

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post