Header ads

Header ads
» » Ngassa Atua YANGA piga Tizi chini ya Van der Pluijm....Mashabiki wapagawa

Winga wa Free States Stars ya Afrika kusini na timu ya Taifa ya Tanzania, Mrisho Ngassa leo asubuhi amefanya mazoezi na klabu yake ya zamani ya Yanga wakati timu hiyo ikiendelea na mazoezi yake kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi Julai.
Ngassa aligeuka kivutio kikubwa kwa mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kushuhudia mazoezi hayo kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, muda mwingi walikuwa wakimshangilia na kuonekana hawaamini kilichotokea. Wengine wakaenda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda mchezaji huyo ameshindwa kufiti kwenye klabu yake mpya na ameamua kurejea nyumbani.




Winga huyo ambaye kwa kiasi kikubwa alichangia mafanikio makubwa ya Yanga msimu uliopita na kuisaidia timu yake kushinda taji la ligi kwa mara ya 25 katika historia ya klabu hiyo. Ngassa alitinga kwenye mazoezi akiwa amevalia jezi za Yanga na alifanya mazoezi chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm akisaidiwa na Charles Boniface Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Juma Pondamali.

Ngassa amesama, watu wasishangae kumuona akiwa mazoezini na klabu yake ya zamani (Yanga) kwasababu hapo ni nyumbani na anarudi muda wowote akijisikia kwasababu hakuondoka kwa ubaya.

Kwasasa Ngassa yupo nchini baada ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichoenda kucheza dhidi ya Misri mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika. Lakini alizuiliwa na shirikisho la soka la Afrika CAF kucheza mechi ya CHAN dhidi ya Uganga kwasababu kwa sasa Ngassa anatambulika kama mchezaji wa kimataifa. Lakini winga huyo ataondoka muda wowote kuanzia sasa kurejea kwenye klabu yake kutekeleza majukumu yake.

Ngassa ambaye amewahi kukipiga kwenye vilabu mbalimbali vya ligi kuu hapa Tanzania akianzia Kagera Sugar, Yanga, Azam FC Simba SC na badae kurejea ten Yanga, aliondoka Yanga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika kwenye klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani mara baada ya kumalizika kwa ligi msimu uliopita.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post