Header ads

Header ads
» » UTAFITI: Watoto Wenye Umri wa Miaka 10 Wanavuta sigara Nchini Uingereza

 
Watoto wenye umri wa miaka 10 wanavuta sigara na kula vyakula vyenye mafuta mengi.
Aidha utafiti uliofanyika Uingereza unaonesha kuwa watoto hao hata wanakunywa vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini kama kiamsha kinywa asubuhi ya siku yao ya mitihani.

Hayo ni baadhi tu ya matokeo ya utafiti wa watoto takriban 1,000 uliogundua kuwa 8 kati yao wanavuta sigara asubuhi ya siku ya mtihani.
Utafiti huo uliofanywa mwaka uliopita uligundua kuwa takriban watoto 37 walikula Chocoleti kama kiamsha kinywa.

Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Opinion Matters ilibaini kuwa asilimia 55% walikuwa wakihofia kuandikisha matokeo duni na kuwa yangeathiri maisha yao ya baadaye.
Uafiti mwengine huru uliofanywa wakati huo huo pia uligundua kuwa asili mia 20% ya wazazi waligundua kuwa watoto wao walishikwa na mhangaiko wakati wa mitihani.
Mzazi mmoja kati ya nane alisema kuwa wakati huo wa kufanya mitihani, wanawao walisusia kula kutokana na hofu.
22% walipoteza usingizi wao mapema kuliko kawaida, 59% walikataa kula wakati wa mitihani huku 74% ya wazazi wakikiri kushikwa na mahangaiko sawa na hayo wakiwa wachanga wenyewe.
 
Hata hivyo mwanasaikolojia wa maswala ya watoto Dakta Claire Halsey anasema kuwa sio jambo la kawaida kwa watoto wachanga hivyo kushikwa na wasiwasi wa mtihani.
''sio kawaida kwa kweli kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 10-11 wanashikwa na hofu katika mitihani yao''.
Mwenyekiti wa shirika linahusiana na maswala ya watoto John Coe amependekeza kuwa watoto wa umri huo wapewe chakula kwa pamoja ilikupunguza shinikizo la matokeo mema.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post