Mji wa Tanga ni
mji mkuu wa Mkoa wa Tanga uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga
ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya kaskazini mwa Tanzania. Njia
ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo niliambiwa na wenyeji wa mkoa huo linamaana ya shamba, wao hulitamka N'tanga.
Tanga ni mji muhimu kihistoria kufuatia kuwa Pangani ilikuwa pia kituo muhimu cha misafara iliyoanza hapa kuelekea ndani ya bara na pia soko muhimu la watumwa.
Baada ya Uingereza
kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani reli ya
Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati hivyo ikawa na njia
kwenda Daressalaam pia.
Mji
wa Tanga una vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango ya Amboni,
mbuga za Saadan, magofu ya Tongoni.Tongoni pamoja na Maeneo ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (Marine Park) kama Maziwe Marine Reserve na zingine nyingi..ipo kilomita 20 kusini mwa
Tanga na mzunu wa kwanza kutembelea eneo hili alikuwa ni Vasco da Gama mwaka 1498.
Tuanze Kutazama Taswira za Jiji la Tanga katika picha.
Hapa nikiwa na Wadau wangu Tukielekea Maziwe Marine Reserve Ambayo ni Kisiwa kilichotengwa kwa Ajiri ya Hifadhi Bahari, Ambapo Watarii wa ndani na Nje Utembelea Eneo hilo
Mitaa ya Tanga
Mitaa ya Tanga
Tanga mjini
Jengo la Cliff lililopo katika hospitali ya mkoa ya Bombo.Jengo hili lilijengwa na wajerumani.
Jengo la mahakama ya Mwanzo ya Usambara ambalo lilijengwa na Wajerumani
Hoteli ya Mkonge
Hoteli ya Tanga Beach Resort
Mitaa ya Tanga
Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanga
Bandari ya Tanga
Jamat,Tanga
Magofu ya Tongoni.Haya ni mabaki ya msikiti katika karne ya 15
Mabaki ya nyumba za waarabu,Pangani | |||||
Mapango ya Amboni ambayo yalikuwa ni maficho ya Osale Otango aliyewasumbua sana wakoloni wa Kijerumani kwa kuwaibia au kuwauwa Kiwanda cha maziwa,Tanga Fresh ambacho kipo Tanga.Kiwanda hiki kinatengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na maziwa kama jibini, maziwa ya mtindi n.k Wilaya ya Pangani ni maarufu kwa kilimo cha nazi Wakazi wa Tanga hujishughulisha na uvuvi.Pichani biashara ya samaki katika soko maarufu la samaki lijulikanalo kama Deep Sea Waachuuzi wa samaki Shamba la mkonge. Mkonge ndio zao la biashara Mkoani Tanga, |