Header ads

Header ads
» » Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba Amejiuzulu Wadhifa huo


Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
----
Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasu hiyo jana Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini Dodoma




Akithibiths tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Naoe Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu

"Mwigulu alishamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC".amesema Nape

Nape amesema kufuatia uamuzi wa mwigulu kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete amemteua Msaidizi wake wa maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kamteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post