Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Meli kubwa zaidi ya abiria duniani iliyoundwa katika karakana ya Saint-Nazaire kusini mwa Ufaransa, imeanza kufanyiwa majaribio bahar...
-
Hapa naongelea zile program zisizotakiwa ambazo zinachukua mamlaka katika vivinjari kama vile Google Chrome na Mozila firefox na ku...
-
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...
-
Siku ya August 11, 2016 Gazeti la Bangladesh Daily Star liliripoti kuwa Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Simu ya Bangladeshi iliamu...
-
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi ...
-
Kuanzia kwenye kufanya manunuzi ya vitu,kuelekezwa mitaa, kuangalia barua pepe na hata kuwasiliana na ndugu pamoja na jamaa. Mambo ya ku...
-
Teknolojia hii imetokea wapi? Huko nchini Japan kuna mahekalu ya kitamaduni ambayo huvunjwa na kujengwa upya kila baada ya miaka 2...
-
Kumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuk...
-
UJERUMANI imetinga Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika...
-
CHANGAMOTO ya kuwaendeleza vijana kitaaluma nje ya nchi imezidi kuongezeka hivyo viongozi ndani na nje ya nchi wapo katika jitihada kut...