Kutana na mtiania wa ubunge mdogo kuliko wote kwenye Historia ya Taifa letu
Arumeru Arusha Wakati tunahesabu miezi kuelekea uchaguzi mkuu 2015,mengi ya kufurahisha yanahibuka kama vile wananchi wa jimbo la Arumeru Magharibi kumshawishi mgombea waokijana Shangwa ole Ikayo achukue fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo 2015,na kummiminia sifa zote zinazofaa kijana huyo wa Arumeru Magharibi achaguliwe.
Wakazi hao wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa sasa wanadai kuwa kijana wao waliomshawishi achukue fomu ndiye Mgombea kijana mwenye umri mdogo kuliko wengine wote wenye nia ya kugombea ubunge Tanzania kwani Bwana Ole Ikayo ana umri wa miaka 21 tu, na hakuna mgombea yoyote hadi sasa mwenye umri chini ya miaka 25 Mwenye nia na Ubunge Wenyewe wakazi wa jimbo la Arumeru Magharibi wanadai kuwa kijana huyo mdogo ndio pendekezo na tumaini lao la uchaguzi 2015,na wanahidi kumpa kila wawezalo bila kujali atagombea kwa kupitia tiketi ya chama gani,wanachojali uwezo wake wa kuwatumikia na kuwawakilisha bungeni.
Kijana Ole Ikayo Jr ni mkazi wa mkoa wa Arusha Na mwanachama wa CHADEMA kama inavyodaiwa na wengi inasemekena ni kijana mwenye mvuto sana kwa jamii kutokana na ukaribu huo na wananchi wa jimbo la Arumeru Magharibi uwambii chochote juu ya kijana wao huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye wamempa majina mengi kama a.k.a Ole Mtetezi wakiamini nfiye Mtetezi wao pekee walienaye na kauli mbiu yao ni "Iwe giza iwe Mvua lazima tumpate kiongozi bora October"
Mytake
Mimi binafsi sina tatizo na vijana kushika hatamu ya taifa hili kwa kua hata Uhuru huu ulipiganiwa na vijana
hata hivyo vijana ndio chachu ya mabadiliko Duniani kote.
lakini je Arumeru imeamua kuongozwa na vijana tu? Tunakumbuka Nassari kwa mara ya kwanza 2010 aligombea akiwa na miaka 24 tu..je chama chake kitampa Nafasi ?
Tusubiri tuone
Note: Uchaguzi ulipita kenya kuna kijana wa miaka 19 alichaguliwa kuwa diwani na uchaguzi ulioisha hivi karibuni Nchini Uingereza kuna Binti wa miaka 20 na mwanafunzi wa mwaka wa pili alichaguliwa kuwa Mbunge je ni wakati wa Ole Ikayo Jr Arumeru Magharibi?
Professor kilaza