Header ads

Header ads
» » Hii Ndiyo Nyuma ya Pazia ya Mkutano wa Mh LOWASSA Wakati Akitangaza Nia Ya Kuomba Kuteuliwa na CCM Kuwa Mgombea Urais Wa Tanzania

 
Asilimia zaidi ya 90% ya watu waliokuwepo uwanjani wamegharamiwa. Bodaboda walilipwa, Wanafunzi walisafirishwa, Waandishi walilipwa. Wachache walioenda kwa hiari yao walienda kushangaa tu wala sio mashabiki wa Lowassa. This is to say ikiwa Lowassa asingetumia pesa huenda uwanjani angekua yeye na familia yake tu.
2. Wengi wanaomuunga mkono Lowassa ni "opportunists". Ni watu wanaotegemea akiingia madarakani awakumbuke. Either awape vyeo au awape unafuu kwenye biashara zao. Hakuna yeyote kwny kundi la Lowassa anayemuunga mkono kwa lengo la kuisaidia nchi.
3. Afya ya Eddo imedhoofu sn na hawezi kuwa Rais wa nchi. Alipoingia uwanjani ameshindwa kupanda ngazi za jukwaa, akasimama katikati ya ngazi kwa dakika chache kabla ya kusaidiwa kupanda. Pia anaongea kwa Shida, na mikono yake haina nguvu. Hali hii imesababisha ashindwe kushika microphone alipopewa "mike" na Kibonde. Mzee Kingunge yupo fit kiafya kuliko Eddo.!
4. Mkutano wa Lowassa leo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Kuna watu wamepata hela ya kulipa mahari kupitia mkutano huu, kuna waliopata mitaji ya kukuza biashara zao na kuna waliopata lift za bure za kwenda Arusha kufanya mambo yao. Hii inaitwa "mbwa kala mbwa"
5. Kutokana na maelezo ya Eddo ni wazi kuwa ana "bifu" na JK. Amekiri kuwa alimpigania sn Kikwete 1995 na 2005 lakini inavyoonekana JK amemsaliti.
6. Akiingia madarakani atalipiza kisasi kwa wabaya wake wote hasa Samuel Sitta, Anthony Diallo na vibaraka wao wote. Ikiwa Eddo atashinda kuna dalili Sitta, Dialo, Makonda, na vibaraka wengine wa CCM wakaishia jela.!
7. Mkutano wa leo ulikua ni mkwara wa kuionesha Kamati kuu ya chama chake kuwa ana nguvu kiasi gani, ili wasijaribu kabisa kukata jina lake wakihofia kukipasua chama.
8. Safari ya matumaini ni safari ya matamanio. Au unaweza kuiita safari ya matumizi. Huwezi kutumia 1.4 bilion for just a single day wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa "padadol" ya shilingi mia halafu ukasema ni matumaini. Labda matumaini ya kuuza nchi.!
9. Ikiwa Eddo atashinda Yuko tayari kutumia rasilimali za nchi ili kulipa fadhila kwa rafiki zake waliomuunga mkono wakati wa kugombea. Kwa mfano yupo tayari kumgawia Mengi vitalu vya gesi Mtwara na kuwaacha watanzania wasinufaike na gesi yao kisa tu Mengi alimpa support kwny kugombea.
10. Lowassa ni msanii mzuri wa sanaa za maonesho. Ametumia makundi yote mawili ktk kufanikisha azma yake. Kundi la Maskini na kundi la matajiri.Ametumia maskini kwa kuwaahidi kuwa atawabana matajiri walipe kodi ili kuboresha maisha ya maskini.
Na ametumia matajiri akiwaahidi kuwa atawabana maskini ili wasipige kelele wakati anawagawia matajiri rasilimali za nchi. Hii ni sanaa. Ha hakika hapa Eddo ameitumia vizuri elimu yake ya sanaa ya chuo kikuu cha Dar es Salaa. (B.A in Fine &Perfoming Arts).!

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post