Header ads

Header ads
» » CCM kwaiva: Kama si Salim ni Mwandosya


Ingawa nipo Arusha,naendelea kudokezwa yanayochomoza vikaoni (ndani ya CCM) na katikati ya makada wa haja. Nimedokezwa kuwa CCM inaelekea kugeukia kwa wanachama wawili ambao kura zao hazikutosha mwaka 2005 na 2010, Dr. Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya. Nikaambiwa kuwa makada hawa wawili wana kila sifa za kuwa Rais wa Tanzania na hawana makuu wala makundi. Pia,wako mbali na kashfa ya aina yoyote iliyoitafuna taifa.




Ninaaminishwa kuwa ripoti mpya ya CAG imempiga mweleka Dr John Pombe Magufuli kwakuwa Wizara yake ililidanganya Bunge na kufisidi mamilioni ya fedha (bilioni 262). Dr. Salim na Prof. Mwandosya sasa wanatazamwa kama dawa pekee ya kuiponya CCM katika kipindi ambacho chama na Serikali yake kimeandamwa na kashfa za kifisadi za kila aina na rangi. Nikaambiwa kuwa Salim na Mwandosya watashawishiwa kuchukua fomu za kugombea kipenga kitakapopulizwa.

Hatimaye CCM yetu imepata pakutokea. Walionidokeza na kuniambia ni wabobezi wenzangu chamani na nawaamini. Afadhali papoe jamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post