Header ads

Header ads
» »Unlabelled » Huyu ndiye Rais Mpya wa Nigeria


Rais mteule wa Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, INEC, Attahiru Jega amemtangaza rasmi Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari kuwa rais wa taifa hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga rais wa zamani Goodluck Jonathan.
Wafuasi wa Jenerali Buhari wakishangilia ushindi huo.
Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha kubali kushindwa kwake baada ya kumpigia simu mpinzani wake, Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.
Jenerali Buhari akiwapungia mikono wananchi na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi.

Hii inakuwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
 

Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo . Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.
 

Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.
 
BBC SWAHILI

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post