Header ads

Header ads
» » Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiasha Nchini Aaachiwa Kwa Dhamana



Habari  Zilizotufikia  zinadai kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiasha nchini Tanzania Bwana Jonson Minja ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma baada ya wafanyabiashara kuweka mgomo ambao ulikuwa haujafahamika ukomo wake.
 
Sakata  hili la wafanyabiashara kufanya mgomo wa kufunga maduka katika mikoa mbalimbali nchini,  jana lilichafua hali ya hewa bungeni baada ya baadhi ya wabunge kuitaka Serikali itoe tamko kuhusu hali hiyo.

Tukio hilo liliibuka bungeni Mjini Dodoma jana baada ya  kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge waliomba  mwongozo ili kuhoji hali inayoendelea nchini dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara kufunga maduka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa, Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, alishangazwa na  kauli zinazotolewa na Serikali kuwa mambo yao na wafanyabiashara yako sawa badala ya kueleza walichojadili na kufikia makubaliano.

"Waziri wa Fedha (Saada Mkuya), amekuwa akihudhuria katika vikao hivyo, kusikiliza hoja zao hivyo tunachokitaka alieleze Bunge hili suala linaloendelea si kusema uongo.

"Mwaka 2014 Serikali iliunda Kamati ya Maridhiano ambayo ilishirikisha wafanyabiashara waweze kukaa pamoja na Serikali kujadili na kufikia mwafaka lakini imechukua muda mrefu kuitisha  vikao ili kujadili kwa pamoja," 
alisema.

Alisema hata wakiitisha vikao hivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara hao hayupo; hivyo itakuwa kazi bure na
kuitaka Serikali iangalie namna ya kumpatia dhamana kiongozi huyo ili vikao hivyo viendelee.
 
Mwenyekiti huyo anakabiliwa  na mashtaka mawili ya kuwachochea wafanyabiashara mkoani Dodoma kutenda kosa na kuwakataza wafanyabiashara nchini wasitumie mashine za kieletroniki za kukusanya kodi za EFDS ambavyo vyote ni makosa ya jinai.
 

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post