Header ads

Header ads
» » Yamoto Band Kuchapa Show Nyingine Muscat.


Milango ya kimataifa inaendelea kuwafungukia vijana wa Yamoto Band, baada ya kuwarusha mashabiki wa London, Uingereza hivi karibuni sasa wamepata show nyingine ya Muscat pamoja na Ommy Dimpoz.

“Kwa sasa hivi Wiki inayofata watakuwa Muscat, watakuwa na bwana Omary Nyembo Ommy Dimpoz wamepata show kule kwahiyo madogo watakuwa na ndugu yao Ommy Dimpo Muscat.”meneja wa Yamoto Mkubwa Fella ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Fella amesema kuwa Yamoto baada ya show ya Muscat watakuwa na ziara nyingine kubwa ya kuzunguka nchi sita.
“Halafu wakirudi wamepata tour moja kubwa ila hatuwezi kuzungumza unajua safari za nje muhimu kwanza kupata visa, ila jamaa mialiko walishaleta kwahiyo wakirudi Muscat ndio tutaanza kuingia kwenye balozi […] halafu tutafahamishana kwamba wataenda nchi gani, lakini hii itakuwa kidogo kubwa manake wataenda tour kama ya nchi sita.” Alimaliza Fella

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post