Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa msaada wa mabati 850 ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kusaidia waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama.Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa (pichani), alisema msaada huo una thamani ya Sh. milioni 12.Dk. Slaa alifafanua kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha zilizonunua mabati, Sh. milioni 10 ni sehemu ya ruzuku inayotolewa na serikali kwa chama hicho na kiasi kingine ni michango iliyopatikana katika mikutano ya hadhara ya chama hicho iliyofanyika mjini Kahama.Alisema waliamua kununua mabati hayo kutokana na kamati ya mkoa inayoratibu maafa hayo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga, kupendekeza vinunuliwe vifaa vya ujenzi kutokana na chakula kuwapo cha kutosha.
Dk. Slaa aliwataka viongozi kuhakikisha wanasimamia vema ujenzi wa nyumba za kuduma za makazi ya wananchi wa kata ya Mwakata kama ilivyopendekezwa na Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea waathirika hao kwani mara nyingi serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza kwa wakati majanga kama hayo.“Niwaombe viongozi wa mkoa kusimamia waathirika hawa wajengewe nyumba kwamuda mwafaka…
Watanzania wengi tanawakatisha tamaa kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zinazotolewa kama kule Kilosa hadi leo bado watu wanaishi kwenye mahema, tangu nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, naomba sana Shinyanga muwe wamfano,” alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, misaada imeendelea kutolewa kwa waathirika hao baada ya Kampuni ya Simu (TTCL), kutoa chakula na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. milioni tatu.Meneja wa TTCL Mkoa wa Shinyanga, Peter Kuguru, alisema kampuni yake imeungana na Watanzania wengine walioguswa na maafa hayo kutoa msaadawa kibinadamu na kuyaasa mashirika mengine na watu mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wananchi hao.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.

Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Kampuni moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom Ship’, itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu ch...
-
MfanyabiAshara ‘alwatani’ Bongo, mkazi wa jijini Dar, Allain Tajiri amekumbwa na skendo nzito baada ya kufumaniwa na mwanafunzi wa s...
-
Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa ...
-
Wanamazingira barani Afrika wamezitaka serikali za nchi za Afrika kuwekeza zaidi kwenye miradi ya teknolojia ya nishati endelevu, ili ...
-
Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani la taifa,Dk Charles Msonde Dar es Salaam. Juhudi za Serikali kuinua ufaulu wa m...
-
Manispaa ya Paris imeanzisha utumizi wa mabasi yanayotumia umeme kusafirisha abiria kwa masafa mafupi. Usafirishaji kwa kutumia mabasi h...
Data Boosta

Ungana nasi Facebook
PPF FUND
