Header ads

Header ads
» » TAARIFA YA MWALIMU ALIYEISHI NA LUNDO LA KINYESI CHA BINADAMU KWA MIAKA (2) NDANI YA CHUMBA CHAKE


Kinyesi kilichokutwa ndani ya nyumba ya mwalimu huyo
Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar es salaam. 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu Gaudensia Missanga mkazi wa Kisiwani kata ya Sandali wilayani Temeke anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi lundo la kinyesi hali ambayo inatishia usalama wa afya yake.

Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje?

  Mwandishi wa habari hizi amefika hadi kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi na kuzungumza na mwenye nyumba Reuben Shayo ambaye ameeleza kilicho sababisha kubaini uchafu huo.

‘’Tuliona funza wakitoka chini ya mlango wake na harufu mbaya ikitoka na mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni ndiyo tukabaini hali hii,’’alisema Shayo.

Kwa upande wake mwalimu Gaudensia anayetuhumiwa kuishi na kinyesi kinachodhaniwa kuwa ni cha binadamu hakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo na alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila majibu.

Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka nyumbani kwa mwalimu huyo chumba chake kilikuwa kimefungwa huku taratibu zingine zikiwa zinaendelea.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post