Header ads

Header ads
» » LOWASSA ANAFAA AU HAFAI KUWA RAIS 2015?

UKITAJA jina la Edward Ngoyayi Lowassa utakuwa unamzungumzia Mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha tangu mwaka 1990 na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliyezaliwa  Agosti 26, 1953.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliyezaliwa  Agosti 26, 1953 Mheshimiwa Lowassa.
Mheshimiwa Lowassa amesoma elimu yake ya msingi katika shule ya Monduli na baadaye Sekondari Arusha (Ilboru) na Milambo mkoani Tabora alikojiwekea mazingira mazuri ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuchukua shahada yake ya kwanza ya masuala…
UKITAJA jina la Edward Ngoyayi Lowassa utakuwa unamzungumzia Mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha tangu mwaka 1990 na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliyezaliwa  Agosti 26, 1953.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliyezaliwa  Agosti 26, 1953 Mheshimiwa Lowassa.
Mheshimiwa Lowassa amesoma elimu yake ya msingi katika shule ya Monduli na baadaye Sekondari Arusha (Ilboru) na Milambo mkoani Tabora alikojiwekea mazingira mazuri ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuchukua shahada yake ya kwanza ya masuala ya tamthiliya na kisha shahada ya pili ya Sayansi ya Maendeleo ya Jamii aliyoipata Chuo cha Hull nchini Uingereza.
Baadhi ya nyadhaifa alizowahi kushika ni pamoja na     Naibu Waziri wa Mazingira na Mapambano Dhidi ya Umaskini, katika ofisi wa makamu wa rais (1988-2000),  Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha ‘AICC) (1989-1990), Waziri Mdogo wa Haki na Mambo ya Bunge (1990-1993), Waziri wa Ardhi na Makazi (1993-1995), Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2005 -2008).
KUJIUZULU KWAKE
Februari 7, 2008, Lowassa alikumbwa na mtikisiko wa sakata la mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambapo kamati teule ya bunge iliyoongozwa na Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ilimhusisha kwenye skendo hiyo inayotajwa kulitia hasara taifa kwa kiasi cha shilingi bilioni 220, mbali na Waziri wa Nishati na Madini wakati huo  Ibrahim Msabaha kuachia ngazi waziri mkuu Lowassa hakusalimika.
Tangu wakati huo yamezungumzwa mambo mengi kuhusu uamuzi huo wa waziri mkuu kuachia ngazi katika mazingira ambayo yalitafsiriwa kuwa huenda yangetikisa msingi wa serikali ya awamu ya nne kutokana na kile kilichoaminiwa na wengi kuwa, rais wa sasa Jakaya Kikwete na Lowassa ni watu ambao hawatenganishwi kisiasa, lakini mambo hayakuwa hivyo.
Hata hivyo, mabadiliko ya baraza la mawaziri baada ya sakata la Richmond yalifanyika kwa utulivu na mambo yakaenda vizuri.Tangu wakati huo Lowassa amekuwa ni mtu mtulivu kinyume na fikra za wengi kuwa huenda ulikuwa ni muda wake muafaka wa kumwaga mboga za swahiba wake Kikwete ili kujiokoa na kivuli cha ufisadi ambacho kilitokana na kashfa ya Richmond.
Duru za kisiasa zinaeleza kuwa ukimya wa waziri mkuu huyo umekuwa na mafanikio makubwa miongoni mwa jamii na wafuasi wake. Francis Kifutumo wa Marine Kigoma anasema: Ukimya wa Lowassa umezizika tuhuma zake.


Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post