Header ads

Header ads
» » YANGA YAMTIMUA KASEJA

Juma Kaseja akifanya mazoezi 


Zanzibar. Hatimaye uongozi wa Yanga umetangaza rasmi kuachana na kipa wake Juma Kaseja wakisema kuanzia sasa ni mchezaji huru. Awali kipa huyo mkongwe aliamua kuipa kisogo timu hiyo akilalamikia kutolipwa sehemu ya fedha zake za usajili pamoja na bima ya afya yake.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema uongozi wao umefikia uamuzi huo baada ya Kaseja kuamua kuvunja mkataba wake kwa kujiondoa katika kikosi hicho.
Muro alisema Kaseja aliamua kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu mfululizo bila ya taarifa kwa waajiri wake kitendo ambacho ni kinyume na sheria za kazi.
Alisema Yanga haidaiwi na Kaseja chochote na kipa huyo aliyesajiliwa kwa miaka miwili Novemba 8, 2013 alilipwa kiasi cha Sh20 milioni wakati akisajiliwa huku kiasi kingine akilipwa mapema mwaka jana kabla ya kuanza kulalamika.
“Katika mkataba wetu na Kaseja hakuna kifungu kinachosema tulitakiwa kumlipa lini hicho kiasi kilichosalia, lakini Yanga tukamlipa fedha zake hata kabla ya kuanza kulalamika,” alisema Muro.
“Ukiangalia barua yake pia Kaseja alilalamika kwamba hapangwi katika timu, lakini kwa mujibu wa makocha waliokuwepo wakati huo walituambia hakuwa na uwezo wa kucheza mechi labda tunampa nafasi katika mechi dhidi ya CDA ya Dodoma na timu moja ya Shinyanga.
Aidha Muro alisema wakati Yanga ikifikia uamuzi huo, uongozi wao unafikiria kufungua madai kwa kipa huyo kwa kutakiwa kuilipa Yanga fidia ya siyo chini ya sh300 milioni kwa kitendo chake cha kujiondoa katika timu yao.
Mwanzoni mwa mwezi huu katika taarifa iliyotolewa na Kaseja kupitia kwa wakili wake, Samson Mbamba ilisema kuvunjika kwa mkataba kati ya Yanga na mteja wetu Juma Kaseja kwa sababu kubwa moja ya uongozi kukiuka kipengele kikubwa (fundamental term) kwa kutomlipa katika muda mwafaka mteja wetu fedha za awamu ya pili ya usajili.
“Hata hivyo ilikuja kubainika kuwa kiasi cha fedha kilichokuwa kikidaiwa kiliwekwa kwenye akaunti ya mteja wetu Oktoba 27, 2014, ikiwa ni takriban miezi tisa au kumi hivi baada ya muda uliokubalika katika mkataba.
“Aidha fedha hiyo ililipwa kwenye akaunti bila taarifa kwa mteja wetu kama ambavyo ingetakikana na baada ya  kugundua kuwa uongozi wa Yanga uliamua kuupa tena uhai (specific performance) mkataba uliokwishavunjwa tangu Januari  15, 2014 na kuhalalisha upya tena kwa kumlipa fedha za usajili iliyokuwa ikidaiwa.”
Hata hivyo, jana Mwanasheria Mbamba  alisema hawezi kulizungumzia  jambo hilo mpaka pale atakapoonana na mteja wake.
“Siwezi kusema chochote mpaka nitakapokutana kwanza na Kaseja, si unajua tunafanya kazi kwa maelekezo.”

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post