Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari
jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze,
katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze katika viwanja vya
miembe saba polisi. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo
hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama.
Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa
Ridhiwani
pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo.
Kutoka kulia ni Alhaji Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula
Ridhiwani
9katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo
Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze jana
Mbunge
wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea
Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki
kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi
alichochaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi
kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo,
ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja
na zahanati