Header ads

Header ads
» » MWANAMKE WA KWANZA MWEUSI ATEULIWA KUWA MWANASHERI MKUU NCHINI MAREKANI


Loretta Lynch ateuliwa kuwa mwanasheria mkuu nchini Marekani,

Ikulu ya white house nchini Marekani inasema kuwa rais Brack Obama amemteua mwendesha mashtaka wa mji wa New York Loretta Lynch kuwa mkuu wa sheria nchini humo.
Msemaji wa ikulu ya white house alisema kuwa mkuu huyo mpya wa sheria atateuliwa rasmi leo Jumamosi.
Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na bunge la seneti Loretta Lynch atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya afrika kuwa mkuu wa sheria nchini marekani .
Uteuzi huo unafanyika wiki sita baada ya kujiuzulu kwa Eric Holder ambaye ndiye M'marekani wa kwanza mweusi kuteuliwa kuwa mkuu wa sheria nchini humo.

PICHA NA BBC

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post