Jopo
la madaktari katika hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa
kushirikiana na polisi wamefanikiwa kumnasa mkazi wa jijini
Dar-es-salaam Bw Godlove Sozigwa akituhumiwa kuomba kufanya mazoezi ya
kutibu kwa muda kama daktari wa magonjwa ya moyo na figo kwa kutumia
vyeti bandia wakati akitambua kuwa yeye si mtaalam wa tiba.Bw
Godlove Sozigwa kabla ya kukamatwa kwake asubuhi kufuatia jopo hilo la
madaktari kubaini kuwa vyeti alivyoviwasilisha katika hospitali hivyo
julai 31 ni bandia na hata hivyo alipoitwa na kufanyiwa mahojiano amedai
huku akionyesha ukomavu wa kujieleza taaluma hiyo aliipatia katika chuo
cha sayansi, tiba na utafiti cha Muhimbili na kufuzu hata hivyo
alibahatika serikali kumpeleka nchini India kwa mafunzo zaidi kusomea
dawa zaidi.
Kwa
upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani Manyara Dr
Peter Mshali akizungumza na EATV baada ya kukabidhiwa kwa polisi ili
kufanyiwa upelelezi amesema katika mahojiano na jopo la madaktari
walibaini vyeti hivyo ni bandia aidha pia mtuhumiwa Dr huyo Godlove
Sozigwa si mtaalam kulingana na maelezo yake bali ni tapeli na hatari
endapo angebahatika kupata nafasi hiyo.
Naye
kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Deusdedit Nsimeki amekiri na katika
mahojiano amesema polisi imebaini baada ya kumfanyia mahojiano na
upekuzi kumkuta na kompyuta mpakato(laptop) muhuri wa kuchonga wa
hospitali ya rufaa ya Muhimbili, koti na vyeti mbalimbali, lakini
wanafanya upelelezi zaidi kabla ya kumfikisha mahakamani.
Tangu
awali EATV ilishughudia mtego huo mapema asubuhi na baada ya mtuhumiwa
Godlove Sozigwa kufikishwa polisi amekiri kuwa yeye si daktari aliyesoma
chuo hicho cha Muhimbili bali anafanya hivyo kutokana na mazingira
magumu, hasa kwa kuipenda taaluma ya udaktari baada ya kujifunza katika
kituo cha tiba cha Neptune cha matabibu ya kichina kilichopo Ubungo
Plaza jijini Dar-es-salaam na kupata uzoefu