Header ads

Header ads
» » SHEKHE MKUU ATANGAZA SWALA YA IDD KITAIFA KUFANYIKA DAR


  Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao maalumu katika Ofisi za  Mkoa wa Dar es Salaam za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) hii leo, Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo sambamba na hotuba mbalimbali inatarajiwa kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo inatarajiwa kuwa siku ya Jumatatu Julai 28 au Jumanne  Julai 29 mwaka huu.
Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa Kiislamu na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika saa 9 Alasiri katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni Rasmi wa Baraza hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post