Header ads

Header ads
» » HATARI:WATANZANIA 50 KUNYONGWA CHINA KWA DAWA ZA KULEVYA

 Shehena ya dawa za kulevya.


 Mtuhumiwa wa dawa za kulevya akiwa amefungwa kabla ya kupigwa risasi mpaka kufa.
 Watuhumiwa wa dawa za kulevya wakiwa katika eneo ambalo ni maalum kwa kupigiwa risasi mpaka kufa.
Huko China wauza dawa za kulevya wanapigwa risasi namna hii, tena hadharani.

Zaidi ya Watanzania 50 wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Idadi hiyo ni kati ya Watanzania 403 wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali kwa tuhuma hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi ametaja baadhi ya nchi ambazo Watanzania wanashikiliwa kuwa ni Kenya, Uganda, Botswana, Malawi, Msumbiji, China, Brazil, Marekani, Pakistan na Uturuki.
Serikali ya Tanzania imekamilisha muswada wa sheria ya dawa za kulevya ambao ikiwa utapitishwa bungeni utasaidia harakati za kupambana na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia mwezi Januari mpaka Juni mwaka huu, kiasi cha kilo 220 za dawa za kulevya aina ya Heroine na watuhumiwa 18 walikamatwa pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa sambamba na watuhumiwa saba.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post