Wakati
 macho na masikio ya dunia yote yakiwa kwenye soka hasa kwa kipindi hiki
 cha kombe la dunia sasa inshu imekuwa tofauti kwa kampuni ya Beats by 
Dr.Dre ambayo headphone zake zimepigwa marufuku kutumika kwenye kombe la
 dunia.kampuni ya Beats Electronics ilitoa tangazo la luninga lililokuwa
 na dakika 5 ambalo walilipa jina la ‘Tittle the Game before the 
Game’.Katika tangazo hilo wapo mastar kadhaa wa mpira wa miguu kwa msimu
 huu akiwemo mchezaji nyota toka Brazil Neymar Da Silva Santos 
Júnior,Mchezaji wa Spain  Francesc “Cesc” Fàbregas pamoja na mchezaji 
kutoka Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz pamoja na Lil Wyne.Unaambiwa 
baada ya FIFA kuliona hilo tangazo wamewakataza wachezaji wote kuvaa 
headphones hizo za Beats by Dre wakiwa kwenye viwanja hivyo vya kombe la
 dunia pamoja na sehemu zote za sherehe zitakazowahusisha pia waandishi.
Dili 
limeidondokea kampuni ya Sony ambao ni Official Partner na FIFA ambao 
wameahidi kuwapatia wachezaji hao headphones za kuvaa kwa kipindi hicho 
cha kombe la Dunia na hawataruhusiwa kuvaa aina nyingine yoyote ya 
headphone.