Header ads

Header ads
» » Mwizi wa vifaa vya magari anusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali jijini Dar.



MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Juzi  alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake , alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.

“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.

Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.

Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka naye chini.

Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.

Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.

Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.

“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila nawafahamu,” alisema Mbaga.

Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.

Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.

 
 
 
 
 
 
 
 

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post