Header ads

Header ads
» »Unlabelled » KITALE: NAJISKIA VIBAYA SANA KUTOKANA NA MIMI MWENYEWE NI MUISLAMU SAFI NA SIO TEJA KAMA NINAVYOIGIZA

  • MTU WAKE WA KARIBU AINGIA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK
  • NA KUANDIKA MANENO MACHAFU SANA YENYE KUKASHIFU DINI YA KIISLAMU
  • MWENYEWE AOMBA RADHI KWA WATU WOTE

Muigizaji mchekeshaji marufu nchini, "Kitale" amesikitishwa sana na kitendo cha mtu anaemdhania kuwa ni mtu wake wa karibu, kuvamia akaunti yake na kuingia katika ukurasa wake wa facebook na kuandika maneno yenye lugha chafu sana na yenye uchochezi mkubwa wa kidini. (siwezi kuiandika sms hiyo)

licha ya kuandika maneno hayo , mtu huyo ambae anaonekana kuwa na hasira na kisasi kikubwa na Kitale, amethubutu kuandika meseji  yenye kusisitiza kulaaniwa kwa Kitale kwa kile alichokiandika na kuisambaza kwa watu huku akimsisitiza anaeisoma kuituma kwa watu 10.
baada ya kuandikwa kwa sms hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook Kitale anasema alishtuliwa na mshkaji wake ile "oya mbona umeandika hivyo kwenye facebook" ndio alipoingia akakutana na messeji hiyo na kushangaa na ndipo alipoamua kuwafahamisha watu na kuomba msamaha kupitia ukurasa huo huo akiwa ameandika yafuatayo
Kitale Rais Wa Matejah

Tuesday.Assalam Aleykum kwa wale WAISLAM NA WASIOKUA WAISLAM, SAMAHAN SANA NDUG ZANGU KUNA MTU AMEFANYA HIK KITU PASIPO MWENYEW KUJUA NA BAADA YA KUPGIW SIM NA MASHABIK WANGU KUA KUNA KITU KAMA HIKI NMEJCKIA VBAYA SANA KUTOKANA NA MM MWENYEW N MUISLAM SAFI NA CO TEJAH KAM NNAVYOIGIZA, HIVYO NAOMBA RADHII NDUG ZANGU..!! HATA PIA HUY MTU ALIKUA ANAWATUMIA WA2 MESSAG KWENY INBOX KUAAMBIA KWAMB NPO DAR, NAWATHIBTISHIA KWAMB MM N KITALE NA SAS NPO KAHAMA...!!!

Jamani mambo ya kidini tusiyachukulie mchezo, kulipizana kisasi kuwe na mipaka, angalia madhara ya unachokiandika na kukifanya katika mitandao ya kijamii, ni rahisi sana kushawishi watu na kusababisha maafa, chunga sana na faikiria mara mbili kabla hujaamua kuandika chochote katika mitandao ya jamii iwe facebook, twitter wala instagram.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post