Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wasanii gani ambao watapata nafasi ya kuperfom katika sherehe za kuapishwa Kwa Raisi mpya wa Kenya, Uhuru Kenyata, huku wengine wakitoa majina kama Jaguar ambae pia alikua akimpigia kampeni katika mbio za uraisi na wengineo, jana imetoka list ya wasanii wa Kenya ambao wamekula shavu siku hiyo ambao ni Band ya wavulana tupu "Sauti Souls" mwimbaji wa gospal Rufftone na sarakasi dancers.
Event hiyo ambayo itahudhuriwa na viongozi kibao na kuonyeshwa katika vituo vikubwa vya habari duniani, itafanyika katika viwanja vya Kasarani.
Wakati wa sherehe hizo, Raisi mstaafu Mwai Kibaki atakabidhi katiba pamoja na upanga kwa Kenyata kama saini ya power, na baadae jeshi la Kenya kupiga mizinga 21kuashiria kuwa Kenyata ndio amirijeshi mkuu wa Kenya.