masaa kadhaa baada ya kuachia single
yake mpya "girls" akiwa amemshirikisha Too short, Kid Cud ametangaza
rasmi kutokuwepo katika familia ya kimuziki iliyo chini ya Kanye West.
swala hili licha ya kuwa ameamua
kutangaza sasa, lakini mashabiki walishaanza kushuku na kuuliza
inakuwaje kwenye album yake hakuna mtu alieshirikishwa kutoka katika
familia ya G.O.O.D. Wakati alipokua akifanya interview na Yesi Ortiz ad
DJ Felli Fel, Cudi
alishangaza wasikilizaji alipotangaza kutokuwa mmoja katika lebo
inayoongozwa na Kanye
Kanye anaelewa kwasababu wote tunajaribu
vitu vipya kama wasanii, sasa hivi Cudi anageukia katika record label
yake " Wicked Awesome " na kumnyanyua msanii wake na rafiki King
Chip.akijua kwamba anataka kuondoka kwa takriban miezi sita iliyopita,
Cudi alisema kuwa alimfata manager wa Kanye Don C pamoja na Jay Z
kuwaeleza fikra zake, na wote walimuelewa na kumshauri amuambie tu
Kanye
"kila kitu kiko poa, na amani ipo kwa kila mtu kwenye lebo, lakini natangaza kutokuwepo, mimi na Kanye West tiliongea kwenye simu hiyo siku, na kulikua na kitu nilitaka kumuambia , kuhusu mimi kutaka kuanzisha njia yangu mwenyewe, na alinielewa, na kuniambia " poa kabisa yaani freshi". hii ni katika biashara tu, hakuna bifu lolote na mtu yoyote kutoka kwenye lebo hiyo