Kutokana na utafiti uliofanywa na timu nzima ya www.thechoicetz.com,
imebaini wasanii 6 upande wa muziki wa kizazi kipya wanaoheshimika sana
Tanzani katika jamii.Vigezo vilivyo zingatiwa katika utafiti huu ni
pamoja na kutobaini skendo za ajabu ajabu kwa hawa wasanii,pia hutumiwa
katika utoaji nasaa mbalimbali katika jamii pia wanajiheshimu katika
mambo yao kwa ujumla.
1.LADY JAY DEE
1.LADY JAY DEE
Mwanadada JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii
anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi kubwa ya watu walio
hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye kuheshimika sana
tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya
2.PROF J
Prof J naye hakuwa nyuma katika kutajwa na idadi kubwa,Prof j kama
muhasisi mkubwa wa huu muziki wa kizazi kipya anaheshimika sana kutokana
na mchango wake mkubwa katika hii gemu bila ya kuwa na sifa mbaya
zinazo weza kumchafulia heshima yake
3.FID, Q
Huyu ni msanii aliyezungumziwa kuwa ni mpole sana mkinywa na hufanya
kazi zake kwa umakini mkubwa,Ni mtu apendaye kufikiri jambo kwa umakini
sana kabla ya kulitenda,Pia kazungumziwa sana na idadi kubwa ya walio
hojiwa
4.A.Y
AY kati ya mchakalikaji mkubwa na mpenda maendeleo katika kazi zake, ni
kijana anaye ibeba nembo ya Tanzania katika ngazi ya
kimataifa,Kujiheshimu kwake na kuto kuwa na skendo pamoja na kuchakalika
kwake kunamfanya aonekane kuwa mtu wa kuigwa kwa vijana wengine.
5.MWANA FA
5.MWANA FA
Binamu ama waweza sema pacha wa A.Y kutokana na kuwa na urafiki wa
karibu sana na wa muda mrefu na A.Y.mWANA FA pia katajwa kwa idadi kubwa
ya wadau kama mtu anayeheshimika sana nchini hasahasa katika nyanja hii
ya muziki wa kizazi kipya.
6. JUMA NATURE
Juma Nature ama kiroboto, ni mtu asiye penda makuu pia kazungumziwa kama
mtu anayependa kuona watu wote wakiwa sawa na hapendi kuona manyanyaso
kwa watu wengine sababu ya kuto kuwa na uwezo.Wamemtaja kama mtu mwenye
nyota ya kupendwa sana na watu kwani yaonyesha anaweza akakaa hata
miaka kadhaa bila ya kutoa wimbo wowote ila pindi apandapo tu jukwaani
watu hufarijika hata aimbapo nyimbo za zamani.