MMOJA wa majeruhi wa milipuko wa mabomu ya Mbagala uliotokea miaka miwili iliyopita na kubaki na vipande vya mabomu mwilini, Jenifa Msigwa, amefariki dunia.
Jenifa ambaye vipande hivyo vilimsababishia mwili kupooza kuanzia kiunoni mpaka miguuni alifariki Aprili 8 mwaka huu baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani. Marehemu amezikwa jana katika makaburi ya Mburahati baada ya mwili wake kuagwa nyumbani kwa baba yake Urafiki jijini Dar es Salaam.