
Kampuni ya Facebook hivi karibuni imetangaza kuwa imefanikiwa kufanya
majaribio ya kwanza ya ndege isiyo na rubani iitwayo Aquila inayotumia
nishati ya jua.
Hivi sasa watu bilioni 4 hivi duniani bado
hawajaunganishwa na mtandao wa Internet. Mwaka 2014, kampuni hiyo
ilianzisha maabara ya uunganishaji, ambayo inalenga kutoa huduma ya
mtandao wa Internet kupitia ndege zisizo na rubani, satilaiti na mifumo ya mawasiliano ya simu
Tarehe 28 maabara hiyo ilifanya majaribio ya kwanza ya ndege ya Aquila
huko Arizona, Marekani. Kiunzi cha ndege hii kilitengenezwa kwa nyuzi za
kaboni, upana wa mabawa yake ni mkubwa kuliko ndege ya abiria ya Boeing
737, lakini uzito wake ni theluthi moja ya gari la nishati ya umeme.
Ndege hiyo inaweza kuruka angani kwa miezi mitatu mfululizo, lakini
inatumia nishati chache tu ambayo ni sawa na nishati inayotumiwa na
vyombo vitatu vya kukausha nywele au maikrowevu moja.
Kwa mujibu wa
mpango, ndege hiyo inaweza kuzunguka eneo lenye kipenyo cha kilomita 97,
na kutoa ishara ya mtandao wa Internet kutoka anga yenye urefu wa
kilomita 18 kwa mifumo ya mwangaza leza na mawimbi ya masafa ya
milimita.
Chanzo: technewstoday.com
Home
»
HABARI TECH
» Facebook yafanikiwa kufanya majaribio ya ndege isiyo na rubani inayotumia nishati ya jua
Topics: HABARI TECH
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Kampuni ya Google imetambulika kuwa bidhaa yenye thamani zaidi kwa mujibu wa shirika la fedha la linalojihusisha na ukaguzi wa thamani ya...
-
Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha z...
-
Matukio mengi yan a endelea kutokea yakiusishwa na Wanafunzi kutumia vibaya Mitandao ya Kijamii. Hii ni pamoja n a Wanafunzi wanne wa C...
-
Matumizi mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija, kampuni moja ya te...
-
Baadhi ya watendaji wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ni miongoni mwa...
-
Watu waliojihami wameteka idadi ya watu wasiojulikana katika moja ya maduka makubwa mjini Nairobi leo. Watu 20 inaarifiwa wameuawa...
-
MATUKIO ya ukatili wa kutisha yanazidi kushika kasi kila kona ya nchi, safari hii h...
-
Tuko hospitali ya mkoa wa Njombe muda huu.Mimi Niko kichochoroni nimejibanza baada ta kuanza kupigwa mabomu na polisi. Wananchi walifunga nj...
-
Wanafunzi 7 wa kitivo cha uhandisi wa mashine cha chuo kikuu cha Uludag nchini Uturuki wamefanikiwa kuunda gari la kutumia nishati ya ...
-
Serikali ya Kenya imetangaza mpango wa kuingiza nchini sheria ya kimataifa ya mitandao kwa ajili ya kuimarisha usalama . Idara ya u...
Data Boosta